Swahili / Kiswahili
Je, unazingatia kurudi katika nchi yako ya asili?
Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) linatekeleza utaratibu wa kurudi ambayo hutoa mipango ya usafiri kwa watu ambao wanataka kurudi kwa hiyari kutoka Ufini hadi nchi yao ya asili. Pamoja na mipango ya usafiri, makwao wanaweza kupokea misaada ya fedha kuanzia hundi taslimu €200 hadi €1,500 kwa mtu mzima na €100 hadi €1,000 kwa mtoto ili kusaidia kushirikishwa tena katika jumuia zakurejea. Kwa mbadala, mradi unaweza kutoa kiwango cha juu cha usaidizi wa huduma, kama elimu, vyombo au mafunzo ya utaalamu.
Ni nani anaweza kupata usaidizi chini ya utaratibu wa IOM?
Unaweza kutuma maombi ya kurudi kwa hiyari kama wewe ni mkimbizi wa kutafuta hifadhi Ufini ama kama wewe umeshapokea ulinzi wa uhifadhi au kama kibali cha makazi yako haitumiki tena na unahitaji usadizi wa fadhila ya kurejea wa . Kama maombi yako ya hifadhi bado yako katika mchakato unahitajika kuliondoa ili kurejea na kupokea usaidizi chini ya utaratibu huu. Haustahili kama wewe ni raia wa nchi za jumuiya za ulaya, na ikiwa umepewa uraia wa Ufini.
Kama uko kwa hali pweke, kwa mfano wewe ni mtoto ambaye haukuandamana na mtu, una hali dhati ya matibabu au wewe ni mwathiriwa wa ulanguzi wa binadamu, ni muhimu kuwa uonyeshe haya katika fomu ya ombi. Taarifa hii ni muhimu wakati wa kupanga mipango ya kusafiri na kuungana tena.
Jinsi ya kutuma maombi?
Ni lazima ukamilishe fomu ya kutuma maombi ya Kusaidiwa Kurejea kwa Hiyari na fomu ya maombi ya masaada ya IOM kwa ajili ya usaidizi wa kushirikishwa tena. Katika fomu ya kutuma maombi kwa ajili ya usaidizi wa kushirikishwa tena ni lazima uonyeshe jinsi unakusudia kutumia usaidizi wa kushirikishwa tena baada ya kurejea. Maombi yote yanatayarishwa kibinafsi na IOM, ikizingatia hali yako yote nchini Ufini na ombi ambalo umewasilisha.
Unaweza kupata fomu ya maombi kutoka kwa:
• Mfanyikazi wa huduma ya kijamii katika kituo cha manispaa au kituo cha mapokezi.
• Kituo cha polisi cha mtaani
• Afisi ya IOM iliyoko Helsinki (Maelezo ya mawasiliano yapatikana hapo chini)
• Mradi wa tovuti www.assistedvoluntaryreturn.fi
Fomu zilizokamilishwa na kutiwa sahihi zinapaswa kurudishwa kwa IOM Helsinki ambao wataitayarisha ombi na kukuarifu kuhusu kustahiki kwako. Kama ombi lako litakubaliwa, IOM Helsinki itaanza mipango ya usafiri kwa mashauriano na wewe.
Utafiti wa IOM katika vyombo vya habari
IOM katika mradi huu pia itafanya jitihada kukusanya habari kuhusu vyombo vya habari vilivyotumika kwa uwezekano wa watu wanaorejea kupitia kidadisi kilichotengwa. Habari hii itatumika tu na IOM kukuza huduma zetu inayohusiana na ombi la makaazi nchini Ufini kwa watu wanaorejea kwa hiyari na si kwa lazima. Habari zote zilizokusanywa zitakuwa za usiri na utajaza kidadisi bila kuandika jina lako.. Kama hautaki kabisa kujibu maswali yoyote kuhusu vyanzo vya habari, una uhuru wa kusema la.
Mradi wa IOM inafadhiliwa na Hazina ya Kurejea ya Jumuiya ya Ulaya na Huduma ya Uhamiaji ya Ufini (Migri).
YHTEYSTIEDOT